Pearl Business

Endesha biashara yako kutoka kwenye gumzo.

Pearl Business inageuza ujumbe wa wateja kuwa kikasha kimoja ambacho timu yako inashiriki, kisha inaongeza katalogi, miadi, kaunta, hesabu na tovuti. Vyote ndani ya programu ambamo wateja wako tayari wanazungumza.

Kikasha cha biashara chenye mazungumzo ya mteja yanayojibiwa na timu

Kikasha cha timu

Kikasha kimoja kwa timu yako yote.

Wateja wanaiandikia biashara yako, si yule aliyewapa namba yake. Mpe mtu gumzo, mwachie mwenzako dokezo na ujibu kwa majibu yaliyohifadhiwa. Tafsiri inafanya kazi hapa pia, kwa hiyo unaweza kuwahudumia wateja kwa lugha 20.

  • Kukabidhi, lebo na madokezo
  • Ujumbe wa kukaribisha na wa kutokuwepo, pamoja na saa zako za kazi
  • Kila mwanatimu ana ufunguo wa timu, na gumzo za wateja hufungwa kwa ufunguo huo

Duka

Kaunta inayofuatilia stoo yako.

Rekodi mauzo, pokea bidhaa zilizorudishwa, hesabu stoo na uendeshe zamu kwenye kishikwambi au simu. Wasambazaji, uhamisho na maagizo mapya yako mahali pamoja.

  • Kikapu, punguzo na stakabadhi
  • Kuhesabu stoo, uhamisho na maagizo mapya
  • Zamu na fedha taslimu

Hesabu

Uhasibu unaorekodi oda zilizolipwa kwa ajili yako.

Hesabu za pande mbili na majedwali kwa biashara. Oda zilizolipwa kwenye gumzo zinaingizwa kwa ajili yako, pamoja na ripoti, ulinganishaji wa benki, na kuingiza au kutoa faili za Excel.

  • Maingizo, leja na ripoti
  • Ulinganishaji wa benki na kufunga kipindi
  • Majedwali yenye fomula, na faili za Excel
Uhasibu, ukionyesha pesa iliyopo, faida ya mwezi huu na maingizo ya karibuni

Pearl Sites

Tovuti unayoihariri kwa kuzungumza.

Pearl Sites inaipa biashara yako tovuti. Iambie Pearl cha kubadilisha, kama “Tuko wazi Jumamosi saa 4 asubuhi hadi saa 10 jioni”, nayo itakuonyesha mabadiliko kwanza. Hakuna kinachowafikia wageni hadi uchapishe, na kutoka ukurasa wowote wanaweza kuanzisha gumzo nawe.

  • Kurasa kwa lugha unazochagua
  • Hakuna kinachoonekana hadi uchapishe
  • Matoleo ya awali unayoweza kurejesha
Mazungumzo ya Tovuti katika Pearl Sites, yenye mabadiliko yanayosubiri kuchapishwa

Kaunta yako

  • Kahawa ya maziwa × 27.00
  • Keki ya lozi3.80
  • Jumla10.80

Tunachohifadhi

  • BfkwNXTasItTALKrjkvswJ7kZuOvde0dpf7bhoetylJFqxzSFVfgSzhyW9qJxwGMq+wAxl6Z
  • ID/duDbfw6LP88KwmjQc712VcKOpjRuufXN96Ppl52i3rqsWQJu6Jwq+f0gT
  • 5ccmNi13sW7vm5MgGHgHOJ1kJMtI6dOHQOqHzhTQlMzob+zRR/Yz

Hatuoni mauzo wala stoo yako.

Unachohifadhi kwenye Duka, Mgahawa na Hesabu husimbwa kwa ufunguo wa timu yako, nasi tunakihifadhi bila kuweza kukisoma. Miadi ni tofauti: tunaona nani aliweka miadi ya huduma gani, na lini. Unachochagua kuchapisha, kama katalogi au menyu yako, kiko wazi kwa umma.

Usalama

Anza bure.

Kuzungumza na wateja ni bure kwenye kila mpango. Pro na Enterprise zinaongeza timu kubwa zaidi na zana zaidi.

Kila programu ina jaribio moja la siku 30 kwa kila biashara. Programu ikiisha muda inakuwa ya kusoma tu, na unaweza kusoma, kuchapisha na kutoa ulichohifadhi wakati wowote.

Tukutane kwenye Pearl.

Isakinishe kwenye simu, kishikwambi au kompyuta yako, au ifungue tu kwenye kivinjari chako na usalimie.